Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani ya ndoa, wanawake
ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa wanaume. Hilo
tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke wakati wa
maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.
Hata hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake ambao hawajawahi kuolewa kabisa)
Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake
wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia muda mwingi
katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume wake. Wanawake
hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini ni muhimu
mwanaume wa kumuoa awe nazo.
Vigezo hivyo huwa hata kwa misingi ya
muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka mwanaume huyo wa
kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua, mtanashati, sauti
nzuri n.k.
Inaweza kuwa kama mzaha na ikaonekana ni kipengele kidogo
sana lakini bado kuna wale ambao anaweza kuwa tayari kuolewa ila hataki
sababu tu huyo mwanaume hafananii vile ambavyo yeye anataka mumewe awe.
Kutaka mwanaume tajiri
Kuna wanawake
ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume
yeyote yule ambaye hana pesa nyingi.
Yupo tayari kuolewa ila si kwa
mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata ikitokea mwanaume ana uwezo
kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado huona huyo mwanaume hamfai
hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi ataishi maisha ya
kifahari.
Hivyo hukazana kusubiri na kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume
ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila kujalisha kama huyo mwanaume
kampita sana umri.
Kutompata Mwanaume Ampendae
Hili
ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani na
haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini
anakupenda pia.
Wengi katika kundi hili huamini kuwa mafanikio ya ndoa
kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata kwenye sababu ya
upendo. Kuna wanawake vigezo vya mwanamme awe
vipi havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa.
Yeye kikubwa
anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na
matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu mwanamke
anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe
basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo
atakapokuwa tayari kuolewa.
Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa (SO SELECTIVE)
Kuna
wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika wala
kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka.
Akija wa
mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na uwezo atatoa
sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi kutafuta
maendeleo.
Akija wa kabila hii, atasema hapana hao wana
tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa kasoro
za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa.
Hatimaye inaweza tokea muda wa
kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji lakini ikiwa hata
wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika soko.
Kujiona ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao ni kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa ni mzuri kiasi kwamba wake
kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na hata wote kumtamani.
Hata
hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamo
wake hujiona ni mzuri mno hakuna mfano kama
yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi hili hufanya kujiona
yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu anatakiwa atambue
kuwa ana bahati sana.
Kitendo hiki hukuza nyodo za hali ya juu ya
mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba wanapojitokeza wanaume kutaka
kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na kiburi.
Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.
Wanawake
wametofautiana mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa katika umri
wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda kuolewa
wakiwa wakubwa zaidi.
Katika kundi hili umri kuwa mdogo hutegemeana,
kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado akajiona mdogo na hali
kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni mkubwa na anafaa
kuolewa.
Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa
na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa.
Anapokuwa na umri ambao
anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo
kwake kuingia katika ndoa.
Maradhi hasa UKIMWI
Hili
kama lilivyo kwa wanaume - Pamoja na kuhamasishwa kwingi na wataalamu
wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza kuwa na
mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana kwa vijana
wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo, hawajaoa/olewa
ama kuwahi kuwa na mtoto.
Wengi sana hukata tamaa na huona ni kheri
kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya hudhoofika zaidi.
Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake
kutaka hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia.
Hilo linafanya vigezo
ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume kumuoa
kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.
Wengi hushindwa
kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa maisha ya
maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya kipi
kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.
Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.
- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake
wenyewe (pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile
kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa
mateso, manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.
-
Kuwa na uwezo sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya
lolote lile ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama
mume kwake anaona kama ni utumwa.
Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake
wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile ya kimwili ya
kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani kufanya mapenzi.
Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni waoga sana
wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu
baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu.
Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa
mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.
No comments:
Post a Comment