Ben Pol amezielezea faida na hasara
za kuondoka kwenye label iliyomtambulisha, MLab huku akisema kwa sasa
hana uhuru wa kurekodi nyimbo nyingi kwa wiki kama alivyokuwa kwenye
label hiyo.
“Sasa hivi sina freedom ya kurekodi nyimbo 3 kwa wiki kwasababu
itabidi upige simu, ufanye booking hata two weeks before, uende
utengeneze beat, unaweza ukarekodi wimbo mmoja miezi miwili au mwezi
mmoja. Lakini kipindi nipo MLab unarekodi nyimbo nne, hizi Maneno,
Nikikupata, Maumivu, ndani ya wiki moja nimerekodi nyimbo tatu kwasababu
una all access ya studio, unaweza ukarekodi hata nyimbo mbili siku
moja, yaani hiyo access ndio nimeimiss sasa hivi,” alisema Ben Pol.
Akizungumzia faida za kuondoka MLab, Ben Pol amesema kwa sasa ana
meneja wake binafsi ambaye ni kaka yake na hivyo mazingira ya kufanya
kazi ni rahisi tofauti na kuwa chini ya uongozi wa label.
“Kunakuwa na mlolongo mkubwa hata kama ikitokea kazi kuona maslahi yake ni adimu sana tofauti na ukiwa unafanya mwenyewe.”
No comments:
Post a Comment