Hidaya Njaidi
Muigizaji wa filamu Swahiliwood anayeuvaa uhusika wa mama katika filamu nyingi, Hidaya Njaidi aliyepata
ajali mwanzoni mwa mwaka huu na kuumia vibaya mkono anaomba msaada wa
matibabu kwani mkono wake umesagika kwa ndani na anahitaji kupatiwa
matibabu zaidi nje ya nchi.Akizungumza na Globalpublishers hivi karibuni, Hidaya alisema kuwa kwa sasa mkono wake unamuuma sana na anachosubiri ni kujua kiasi cha pesa anachotakiwa kutoa na hospitali atakayokwenda kutibiwa kati ya India au Afrika Kusini.
“Wiki ijayo ndiyo nitajua baada ya kurudi Muhimbili lakini ukweli ni kwamba mkono unanisumbua. Hata hivyo, sina pesa za kutosha hivyo naomba watu wanisaidie,” alisema Hidaya ambaye ameng'ara sana na filamu nyingi.
Get well soon Hidaya......
No comments:
Post a Comment