Kufuatia mashambulizi ya kigaidi katika
mall ya West Gate jijini Nairobi, kumekuwepo na uvumi kuhusu mwanamke
wa Uingereza aitwaye Samantha Lewthwaite au ‘White Widow’ kuhusika na
tukio hilo. Jana kulikuwa kumekuwa na picha zilizosambaa katika
mitandao ya kijamii pamoja na kuripotiwa na baadhi ya vyombo mbalimbali
vya habari ikiwemo mtandao wa Mail Online wa Uingereza, za mwanamke
ambaye baadhi ya watu waliamini kuwa ni Samantha Lewthwaite au ‘White
Widow’.
Picha ya mwanamke wa Kenya (kushotio) aliyedhaniwa kuwa ‘White Widow’
Habari iliyokuwa inasambaa ni kuwa
mwanamke huyo aliyedhaniwa kuwa ‘white widow’ alitoroka kwa njia ya
kujifanya kumsaidia mwanamke huyo (kwenye picha hapo juu).
NTV ya Kenya iliamua kusahihisha habari
hiyo kwa kumtafuta mwanamke huyo (kushoto katika picha) na walifanikiwa
kumpata na kuweka taarifa hiyo sawa kwa kukanusha kutokuwa mtu ambaye
watu walimdhania.
Akiongea na NTV Mwanamke huyo
alijitambulisha kwa jina la Henna, na wakati wa tukio alikuwa katika
mall ya West gate na wanae wawili pamoja na dereva wakifanya manunuzi
ndipo ghafla mashambulizi yakaanza. Wakati wa kujiokoa aliamua kuwa
msamaria mwema kwa kumsaidia mwathirika mwenzie aliyejeruhiwa kama
ilivyoonekana katika picha iliyozuwa uvumi wa kuwa ‘white widow’.
Mtazame hapa chini
No comments:
Post a Comment