Na Ezekiel Kitula
MSHAMBULIAJI Mrisho Ngassa wa Yanga,
ameuambia uongozi wake yupo tayari ulilipe Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kitita cha Sh milioni 45 kutoka kwenye mshahara wake.
Ngassa amekubali kitita hicho cha fedha
kitolewe kwa kuwa ana hamu ya kuanza kuitumikia Yanga baada ya kumaliza
adhabu ya kutocheza mechi sita aliyopewa na TFF.
Imeelezwa Ngassa yupo tayari kukatwa katika mshahara wake na kuna taarifa katika Sh milioni 2 kila mwezi, atakatwa Sh 500,000.
Mshambuliaji huyo alisimamishwa mechi
sita pamoja na kutakiwa kurudisha Sh milioni 30 alizolipwa na Simba
pamoja na faini ya Sh milioni 15. TFF ilishikilia msimamo wake kwamba
Ngassa hatacheza hadi atakapolipa fedha hizo za Simba.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga
zimeeleza kuwa, Ngassa amekubali kuhusiana na hilo na alifikia
makubaliano hayo na mwenyekiti, Yusuf Manji walipofanya kikao
walipokutana jijini Mbeya, hivi karibuni.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo jana,
Ngassa alisema: “Sawa, adhabu yangu ya kutocheza mechi sita za
mashindano imemalizika, lakini siwezi kuongelea lolote, mimi ni mchezaji
tu, kazi yangu ni ndani ya uwanja, hayo mengine ya kiutawala ni vyema
yakatolewa ufafanuzi na viongozi,” alisema Ngassa.
Championi Jumatano lilimtafuta Manji ambaye alikiri kuzungumza na Ngassa kuhusiana na masuala kadhaa ya klabu yao likiwemo hilo.
“Mimi ni mwenyekiti, hakuna ubaya
kuzungumza na Ngassa. Tunazungumza kwa ajili ya klabu yetu, hivyo
msubiri akicheza mtamuona,” alisema Manji.
Taarifa nyingine zilieleza kuwa, Yanga
ilikuwa tayari kupeleka fedha hizo leo, lakini ilitaka TFF wakate Sh
milioni 45 katika Sh milioni 70 inazowadai na walikuwa katika mazungumzo
katika hilo.
Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu, Ernie
Brandts, alisisitiza kwamba ana kila sababu ya kumpanga Ngassa kama
atakuwa amerejea katika kikosi watakapoivaa Ruvu Shooting Jumamosi.
“Tuko naye kikosini kila siku, tunafanya
naye mazoezi na tunashirikiana. Kama amerejea na yuko katika afya
nzuri, nitampanga maana ninamhitaji,” alisema Brandts.
Wakati hilo la Ngassa linamalizika,
taarifa nyingine za uhakika zimeeleza Manji alitarajia kukutana na
kikosi kizima cha Yanga, jana usiku.
Mwenyekiti huyo alipanga kukutana na
wachezaji na benchi la ufundi katika hoteli ya Serena jijini Dar ili
kula chakula cha usiku na baadaye kujadili masuala kadhaa kikiwemo
kipigo cha Azam FC na nini cha kufanya baada ya hapo ili kusonga mbele
na ikiwezekana kutetea
-GP
No comments:
Post a Comment