Hivyo, inakupasa kufanya utafiti ili
kubaini ni make up ipi sahihi na haina madhara katika ngozi
yako.Vipodozi au ‘Makeups’ ni urembo unaopendwa zaidi
na wanawake wengi, dhamira yao ikiwa kubadili mwonekano wao
uliozoleleka ili wapendeze.Mara nyingi watu wanapopaka make up tofauti
hujitokeza usoni kutokana na kipodozi hicho kufanya kazi ya kung’arisha
na kupendezesha uso.
Unapofika wakati wa kupaka make up, kwanza
unapaswa kuchagua ni ipi itakufaa na kukupendeza. Swali la kama kipi
kitafaa zaidi kati ya poda au cream, hilo linabaki kwa mhusika kwa kuwa
kila mmoja anapendekezo lake, kutokanana namna anavyopata matokeo
mazuri.
Mambo ya kuzingatia kabla hujapaka make up!
Kwanza jaribu kutafuta make up itakayoendana na
ngozi yako na rangi ya mwili wako. Usipake aina yoyoe ya make up eti kwa
sababu umeiona kwa mwenzio amepaka na amependeza kwani kila mmoja ana
rangi yake na huenda anayotumia mwenzio ikawa na madhara katika ngozi
yako.
Hivyo, inakupasa kufanya utafiti ili kubaini ni
make up ipi sahihi na haina madhara katika ngozi yako. Watu wenye ngozi
za mafuta wanashauriwa kupaka make up ya poda au ungaunga kwani cream
inaweza kuziba vitundu vya hewa katika ngozi ya uso, hatimaye
kusababisha chunusi kuonta.
Kwa walio na ngozi kavu wafahamu kuwa, make up ya
cream haina uwezo wa kukaa muda mrefu katika ngozi, hivyo ikiwa
unahitaji iendelee kuonekana kwa muda usiopungua saa nane ni vyema
ukapaka make up ya poda iliyozeleka na wengi.
Jambo jingine la kutilia msisitizo ni namna ya
kupaka aina zote mbili za make up, inashauriwa make up ya poda au unga
ipakwe kwa brashi zake maalumu, siyo mikono wala kitambaa chochote
ambacho hakijawekwa mahususi kwa kazi hiyo.
Ila kwa upande wa make up ya cream au majimaji,
inapaswa kupakwa kwa mikono na kusambazwa katika uso wote, ili kuwe na
ulinganifu katika eneo hili linalohusudiwa zaid na wanawake.
No comments:
Post a Comment