LAANA...BABA AMBAKA BINTI YAKE NA KUZAA NAE WATOTO.
Aziza Kibibi alikuwa na umri wa miaka minane tu wakati baba yake - Mwongozaji wa Tuzo za muziki za MTV - alipoanza kumbaka.Alipofika miaka 10, somo ambalo Aswad Ayinde alikuwa akimfundisha binti yake 'jinsi ya kuwa mwanamke'
likabadilika na ubakaji wake wa mara kwa mara ukazaa watoto watano
kutokana na makosa ya kujamiiana kwa kisingizio cha kujaribu kutengeneza
damu 'halisi'.Kwa
namna ya ajabu mwanamke huyo jasiri, ambaye sasa ana miaka 35, ameolewa
na anaendesha biashara inayoshamiri ya uokaji, alizungumza hadharani
kuhusu maisha yake ya utoto yaliyojaa kiwewe
wiki hii kwa mara ya
kwanza.Kibibi
alielezea maisha yake ya utoto kwamba yalianza katika hali ya kawaida.
Aliishi na mama yake na baba kwenye ghorofa ya tatu ya jengo moja huko
Paterson, New Jersey, huku babu na bibi yake wahamiaji kutoka Jamaica
wakiishi ghorofa ya chini.
Kibibi
alikuwa akisomea nyumbani lakini bado aliruhusiwa kucheza na watoto wa
jirani. Pale familia yake ilipoongezeka na kufikisha watoto wanane
wakahamia kwenye nyumba kubwa zaidi katika jengo hilo.
Hapo ndipo Kibibi akaanza kukua kiasi cha baba yake kuanza kumtazama kwa jicho la matamanio.
"Aliniambia
nilikuwa wa kipekee. Mwanzoni, ilikuwa ni katika kunifundisha jinsi ya
kuwa mwanamke," alisema. "Wakati huo alianza kuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mimi, aliendelea kutumia nguvu zaidi na zaidi. Pale
nilipoanza kupigana naye, alinipiga. Alinipa vitisho vingi mno."
Baba
yake akaanza kubadilika, na kuitawala mno familia kimabavu.
Aliwahamisha kutoka kwenye nyumba ya babu yao na kuwapeleka kwenye
nyumba nyingine huko Paterson kabla ya kuwahamishia Eatontown huko
Southern New Jersey. Watoto hao walikuwa wakiruhusiwa tu kutazama
televisheni kwa muda mchache mno, na hakuna ambacho kilielezea asili ya
maisha ya familia.
Dawa
za kisasa zilipigwa marufuku katika nyumba hiyo, na alimweleza mkewe
kwamba uhusiano wake na Kibibi ulikuwa katika kumtibia ukurutu.
Kibibi
hakuwa pekee ambaye Ayinde alikuwa akifanya naye mapenzi. Alikuwa na
mwanamke wa makamo - mwanasheria wa Manhattan ambaye alizaa naye watoto
wawili - na pia alikuwa akimdhalilisha kijinsia mmoja wa dada zake
Kibibi.
Alijiita
mzee wa mitala na nabii. Familia yake ilikuwa ikiruhusiwa kumwomba
Mungu lakini wanaweza tu kufanya hivyo kupitia kwake.
"Alisema
dunia ilikuwa ikielekea ukingoni, na angebaki yeye tu na watu wake na
kwamba alikuwa amechaguliwa," mkewe wa zamani, Beverly Ayinde alitoa
ushahidi kwenye kesi moja mwaka 2010. Alisema alikuwa akijaribu
kutengeneza damu yake 'halisi' kwa kuzaa na binti zake mwenyewe.
Pale
mtoto wa kwanza wa Kibibi alipozaliwa bila matatizo, Ayinde alitumia
kigezo hicho kama uthibitisho na kuendelea kumbaka msichana huyo hadi
kumpa ujauzito.
Watoto waliofuatia hawakuwa na bahati hivyo.
Mabinti
wawili waliofuatia waliozaliwa kutokana na baba yake waligundulika na
ugonjwa wa phenylketonuria (PKU) ambao huzuia mwili kuweza kuvunja amino
acid. PKU inaweza kusababisha kuharibika ubongo na kifafa.
Dk
Anna Haroutunian, mtaalamu wa PKU ambaye aliwatibu watoto wa Kibibi,
alisema hakika wamepata ugonjwa huo sababu ya uzao baina ya wazazi wa
nasaba moja.
Katika
miaka hiyo, Kibibi amekuwa akikumbwa na shinikizo la kutoroka. Aliweza
tu kulala sababu ndoto zake zilikuwa nzuri kuliko maisha halisi.
"Nilikuwa
na ndoto ya kukimbia. Niliwaza kuwachukua kaka na dada zangu wote -
mmoja wa dada zangu alikuwa mtoto, na nilikuwa nikimlea - nilikuwa na
mawazo ya kuota matiti na kupata maziwa na kukimbia nao mahali fulani,"
alisema.
Pale
alipokuwa mtu mzima na mmoja wa watoto zake wa kiume alipougua,
hatimaye akapata hamasa kumpeleka hospitalini wakati Ayinde alipokuwa
amekwenda mjini kwa safari ya kibiashara.
Lakini
hakuwa akijua jinsi ya kuongea na madaktari na mfanyakazi wa jamii
akaingia, akaitaarifu Idara ya Vijana na Huduma za Familia.
Pale
Ayinde aliporejea kutoka safari yake ya kibiashara aligadhibika, na
kutishia kumrejesha kwa nguvu mtoto wake kutoka hospitali.
Huduma za Watoto waliingia kabla hajachukua uamuzi huo na kuwaweka katika nyumba tofauti.
Baada ya hapo Kibibi, mama yake na dada yake walimtoroka Ayinde wakati akifanya harakati za kuwarejesha nyumbani watoto wake.
Akipambana
kuwarejesha watoto katika himaya yake pia Kibibi aliwezeshwa, na
kubadili maisha yake baada ya udhalilishaji. Sasa anaishi huko East
Orange, New Jersey pamoja na mumewe.
Alirejea
shule na atamaliza shahada yake ya sanaa kwenye Chuo cha Essex County
mwaka huu. Pia anaendesha biashara yake ya uokaji na siku moja anapanga
kuanzisha mgahawa.
Kibibi
na dada yake mwishowe wameamua kufungua mashitaka dhidi ya baba yao
mdhalilishaji. Walichelewa kufungua mashitaka kutokana na kutokuwa na
uhakika wa athari ambazo zingeweza kuwapata watoto wao.
Ameeleza hadharani stori yake kwa matumaini ya kuweka utofauti kwa wote waliopitia maisha kama yake.
"Badala ya kuwa uzoefu niliokuwanao, pengine hii imeniimarisha. Kile kisichotusambaratisha kinatufanya tuwe imara zaidi."
No comments:
Post a Comment