21 September 2013

JESHI LA WANANCHI LA TANZANIA (JWTZ) YAKANUSHA VIKALI TAARIFA ZILIZOENEA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII KWAMBA JWTZ LIMETOA NAFASI ZA KUAJIRI WATAALAMU

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo  : “N G O M E”                Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo  :                              DSM  22150463  

-----

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa taarifa zilizoenea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi (sms) na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba JWTZ limeanza kuajiri wataalamu Jeshini (Professionals) siyo kweli na halina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia mitandao ya kijamii au kupitia simu za mikononi.

          Kwa kawaida, utaratibu wa kujiunga na Jeshi hutangazwa kwenye Vyombo vya Habari pale ambapo Jeshi linahitaji kuandikisha askari wapya.  JWTZ huelekeza utaratibu wa kuzingatia katika kuwasilisha maombi husika kwa taarifa hii, wananchi wote wanatahadharishwa kuhusu ujumbe huo unaoelekea kusababisha usumbufu kwa wananchi na JWTZ.  Taarifa hiyo haijatolewa na JWTZ hivyo wananchi wajihadhari na yeyote atakayejitokeza kuwarubuni na hatimaye kutapeliwa kwa namna yoyote.
                       
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi

Dar es salaam, Tanzania

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname