KUSHOTO: Laxmi akiwa na mdogo wake, Suman. KULIA: Laxmi akijaribu kuvaa viatu vya watu wazima. |
Amekuwa
akishuhudia rafiki zake wakikua kufikia kuwa wasichana wakubwa lakini
Yadev Laxmi hajabadilika tangu alipokuwa na umri wa miaka mitano.
Anaweza
kuwa na miaka 20 lakini bado ana urefu wa futi 3 na inchi 3 tu, huku
akiwa na uzito wa kilo 3 tu na kuvaa nguo za watoto wa miaka sita.
Mvurugiko adimu wa kinasaba umesababisha Laxmi kukoma kukua miaka 15
iliyopita na amestaafu kuishi kwa maisha yake yaliyobaki kama mwanamke
aliyenaswa katika mwili wa utoto.
Laxmi amepitia miaka kadhaa ya kuonewa na kudhihakiwa lakini anasema
jambo gumu zaidi kukabiliana nalo ni hatima yake iliyokataliwa na hali
yake.
Anakiri amekuwa pia akitishwa na kumwamini mwanaume na hofu ya kudharauriwa katika ndoa.
Laxmi, anayetokea Gurgoan, nje ya New Delhi, alisema: "Wakati
mwingine nafikiri kuhusu maisha ya kawaida ambayo ningeweza kuwa nayo na
inanifanya nijisikie mnyonge.
"Ningeweza kuwa na furaha na uhuru na kufurahia maisha waliyonayo wasichana wengine."
Miaka ya dhihaka na hofu kuhusu kutekwa nyara yamemuacha Laxmi akiwa
na mashaka makubwa kutoka nje peke yake lakini anasema anamudu kuendana
na mapungufu yake hayo kupitia msaada kutoka kwa familia yake.
Mama yake, Parvati, mwenye miaka 52, anamnunulia nguo kumsaidia kuepuka manyanyaso ya kununulia nguo kwenye sehemu ya watoto.
Kaka yake Azad anasumbuliwa na hali kama hiyo lakini akaendelea
kushikilia taaluma yake kama mwalimu na anaamini manyanyaso yamemfanya
kujitahidi zaidi kufikia malengo yake.
Mdogo wake wa kike Suman, mwenye miaka 15, ambaye ana kimo cha kawaida, humchunga Laxmi nje na humsaidia 'kumhamasisha'.
Laxmi anasema: "Sipendi kukutana na watu wapya kutokana na kunichoma wanaponishangaa na kunionea kila wakati."
Lakini anasema kwa kufuata uongozi wa Azad na kwa msaada wa baba yake
Bahadur na mama yake, anakabiliana na hofu zake na kuanza kazi kwenye
duka moja.
Laxmi anasema: "Ninahofia lakini niko imara na nitazishinda hofu zangu zote kwa kufanya hivi."
Fedha hizo zitakuwa muhimu kwa familia yake, ambayo inategemea Rupia
8,000 (Pauni za Uingereza 88) kwa mwezi ambazo baba yake anapata
kutokana na kazi ya ulinzi.
Kipato kidogo cha familia hiyo tayari kimeanza kuandamwa na mfululizo wa majanga.
Hawawezi kumudu fedha zinazohitajika kugharimia homoni za kukuza binadamu kwa ajili ya Laxmi na Azad.
Hali zao zingeweza kuimarika kama wangeweza kupatiwa kabla ya kufikisha umri wa miaka 16 au 17.
Madaktari wanasema baadhi ya matibabu yanaendelea kuweza kupatikana lakini yanaweza tu kufanikiwa kama yatafanyika mapema.
Hatahivyo, licha ya magumu yake, Laxmi amestawi kwenye maomo yake.
Amehitimu sekondari ya juu kwa kupata alama za juu kabisa na sasa anataka kuanza kozi ya kompyuta kwenye chuo kimoja.
No comments:
Post a Comment