KIUNGO John Obi Mikel amefunga bao lake
la kwanza katika Ligi Kuu ya England na kuiwezesha Chelsea kuibuka na
ushindi wa 2-0 dhidi ya Fulham Uwanja wa Stamford Bridge, huo ukiwa
ushindi wao wa kwanza mwezi huu.
Mabao ya Oscar na Mikel kipindi cha pili
yamemaliza ukame wa ushindi ndani ya mechi nne na kuendeleza rekodi ya
Jose Mourinho kutofungwa nyumbani katika Ligi Kuu ndani ya mechi 63 na
ushndi wa kwanza tangu wafungwe na Aston Villa.
Ushindi huo wa 2-0 unamaanisha Fulham
inatimiza miaka 34 bila kushinda Stamford Bridge, Chelsea ikizinduka
baada ya vipigo vya Everton na Basle.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech,
Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Ramires, Mikel, Schurrle/Lampard dk79,
Oscar, Hazard/De Bruyne dk85, Eto’o/Torres dk64.
Fulham: Stockdale,
Riether, Amorebieta, Hangeland, Richardson, Duff/Taarabt dk64, Parker,
Sidwell, Kacaniklic/Tue Na Bangna dk72, Kasami/Rodallega dk85 na Bent.
Ushindi umerudi: Oscar akishangilia bao lake na wenzake
Oscar amefunga bao la kwanza leo Stamford Bridge
Bao tamu sana: John Obi Mikel akifunga bao lake la kwanza Ligi Kuu England baada ya mechi 258
Raha sana: Obi akishangilia bao lake
Raha zimerejea Darajani: Jose Mourinho akishangilia ushindi wake wa kwanza mwezi huu
Amekosa: Darren Bent alipoteza nafasi nzuri ya kufunga wakati timu hizo hazijafungana
Maumivu: Scott Parker akichezewa rafu na Gary Cahill
Hdi chini: Steve Sidwell akimuacha chini Eden Hazard baada ya kugombea naye mpira
Mabao wapi?: Samuel Eto'o kwa mara nyingine ameshindwa kuifungia timu yake mpya
John Terry akiwania mpira wa juu
Branislav Ivanovic akipambana na Pajtim Kasami
No comments:
Post a Comment