MAUAJI ya watu watatu wa familia moja yaliyotokea jijini Mwanza hivi
karibuni yameibua maswali mengi lakini mwisho wa yote, imebainika kuwa
kilichoiponza familia hiyo kukumbwa na mauti hayo ni hiki, Uwazi
limechimba mwanzo mwisho.
Mauaji
hayo yalitokea saa 10 alfajiri ya Septemba 21, mwaka huu katika Kijiji
cha Ihila, Kata ya Buhongwa, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza ambapo
inaaminika kuwa mgeni aliyekaribishwa kwenye familia hiyo ndiye
aliyetekeleza mauaji hayo na alikaribishwa nyumbani hapo bila kujulikana
tabia.
Debora Jonas Luhinga, mtoto wa marehemu ambaye alinusurika katika tukio hilo, alisema kuwa mgeni huyo aliyemfahamu kwa jina moja la Lameck alifika nyumbani hapo Septemba 18, mwaka huu lakini baada ya kutekeleza mauaji hayo alitokomea kusikojulikana.

Debora
mwenye umri wa miaka 12, alidai kuwa siku ya tukio, usiku akiwa
amelala, mdogo wake aitwaye Eliudi aliyekuwa amelala naye aliamka na
kuanza kulia sana.
Alisema alichukua jukumu la kumbembeleza mdogo
wake huyo lakini ilishindikana, ghafla Lameck aliingia chumbani humo na
kumwomba mtoto huyo ili ampeleke chumbani kwa wazazi wake akabembelezwe.
“Kilio cha mdogo wangu kilikuwa kikubwa, mara nikaona mlango
unafunguliwa, Lameck akaingia, akasema kwa kuwa mtoto analia sana nimpe
ampeleke kwa mama ili akambembeleze,” alisema Debora.
Akaongeza kuwa alikubali kumpa Lameck mtoto huyo na kwa vile yeye alikuwa na usingizi mzito aliendelea kulala fofofo.
Akaongeza kuwa alikubali kumpa Lameck mtoto huyo na kwa vile yeye alikuwa na usingizi mzito aliendelea kulala fofofo.
Debora alisema alipoamka kulikuwa kumekucha, akashuka kitandani ili aende nje lakini akakuta mlango umefungwa kwa nje.
“Nilipiga kelele baada ya kukuta mlango wa chumba changu umefungwa kwa
nje, majirani walifika kunifungulia lakini nilipigwa na mshangao kukuta
maiti ya baba ikiwa sakafuni sebuleni tena imetapakaa damu.
“Nikiwa
nimechanganyikiwa niliingia chumbani kwa wazazi wangu, nikashangaa
kumuona mama yangu na mdogo wangu Eliudi wakiwa wameuawa kwa kunyongwa
na miili yao imelazwa chini,” alisema Debora.
Debora alisema
anaamini Lameck ambaye mara nyingi alikuwa akimwona akizungumza na baba
yake ndiye aliyetenda unyama huo. Alisema anaamini mtu huyo wakati
anaingia chumbani kwake kumchukua mdogo wake alikuwa ameshawaua wazazi
wake na aliamua kumtwaa mtoto huyo kwenda kumnyonga ili kilio chake
kisiwafanye majirani wakafika nyumbani hapo kutaka kujua kulikoni na
hivyo kugundulika alichokifanya kwa muda huo.
Alikwenda mbele zaidi kwa kusema anaamini baba yake ndiye aliyeanza kuchinjwa kabla ya mama yake kunyongwa.
Alikwenda mbele zaidi kwa kusema anaamini baba yake ndiye aliyeanza kuchinjwa kabla ya mama yake kunyongwa.
Baadhi ya majirani waliozungumza na gazeti hili huku wakiomba majina
yao kuhifadhiwa baada ya tukio hilo, walisema kwa nyakati tofauti kuwa
huenda mauaji hayo ni ya kulipiza kisasi kwa mwanaume huyo ila mkewe na
mtoto waliingizwa kwenye mkumbo tu.
Walisema haiwezekani watu wa familia moja wakauawa kikatili namna hiyo bila ya wauaji kuanika sababu.
Walisema haiwezekani watu wa familia moja wakauawa kikatili namna hiyo bila ya wauaji kuanika sababu.
Waliongeza kwa kudai kuwa siku zote tatu alizoishi hapo, Lameck alikuwa akitafuta njia mwafaka ya kutekeleza ukatili huo.
Walisema mauaji mengi ya aina hiyo yanayotokea katika maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza huhusishwa na imani za kishirikina,
migogoro ya ardhi au mirathi.
Majirani hao waliongeza kuwa awali walikuwa wakimwona Lameck nyumbani kwa marehemu bila kujua uhusiano wao, wakaonya kuwa ni hatari sana kumkaribisha nyumbani mtu usiyemjua kwa undani kama ilivyokuwa kwa Lameck.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,
ACP Ernest Mangu alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo huku akisema
hakuna aliyekamatwa. Aliwataja marehemu kuwa ni Jonas Luhinga, mkewe
Rusia Jonas na mtoto wao, Eliud Jonas.
No comments:
Post a Comment