03 August 2013

HII NDO KAULI YA ROSE NDAUKA BAADA YA HABARI KUENEA KUWA ALIINGIA GESTI NA MSANII WA BONGO FLAVA

Mwanadada Rose Ndauka amewawakia baadhi ya waandishi wanoandika habari zauongo kuhusu yeye kufuatia hivi karibuni kuripotiwa kuwa amekutwa kaitika nyumba ya wageni akivunja amri ya sita na mwanamziki mmoja wa muziki wa kizazi kipya.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii Rose aliandika

“Dah magazeti yanapenda chokochoko kweli haswa wakimuona mtu katulia....kama hujui uliza sio tu unaongea au unaandika kitu ambacho ukijui......mnaudhi sana”

Huku akionesha picha ya gazeti moja la udaku lilikouwa na habari hiyo.



Hapo awali iliripotiwa na baadhi ya mitandao ya habari na baadhi ya magazeti kuwa mwanadada huyu alionekana akipapaswa ndani ya gari na baadaye yeye na mwanamuziki huyo aliyotajwa kwa jina la dogo  Nasry kwenda kuvunja amri ya sita katika hoteli ya chumba hicho.

Source:Bongo Movies

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname