Eto'o akiwasili London (HM)
Chelsea inakaribia kumsajili
mshambuliaji Samuel Eto'o kwa dili la mwaka mmoja lenye thamani ya
£7million kwa mkataba wa mwaka mmoja leo Alhamisi baada ya kukiri
kushindwa kumpata mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney.
Eto'o, 32, amekubali kupunguza dau lake alilokuwa akilipwa na Anzhi kiasi cha £17m kwa mwaka na sasa atasaini atasaini akiwa huru.
Pamoja na hilo, lakini inaeleweka
kwamba Anzhi wamemlipa Eto'o millioni kadhaa ili kuweza kumuondoa katika
listi wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ndaniya klabu ya Anzhi.
Eto'o aliwasili jijini London jana usiku na anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya mchana wa leo katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea Cobham. Chanzo: Shaffihdauda
No comments:
Post a Comment