
Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale,
lakini hili la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi ndiyo
tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo
Kikuu.”
Dar es Salaam. Ofisa mmoja wa Usalama
wa Marekani (FBI), akiwa na mbwa jana aliingia Makao Makuu ya Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam na kufanya ukaguzi.
Tukio hilo lilitokea muda mfupi kabla
ya msafara wa magari ya Marekani kupita yakitokea Ikulu kwenda Uwanja
wa Ndege wa Julius Nyerere kumlaki Rais Barack Obama.
Polisi ambaye hakutaka kutajwa alisema ofisa huyo aliingia na mbwa hadi maeneo ya mapokezi, lakini muda mfupi walitoka.
“Walikwenda moja kwa moja mapokezi
wakafanya ukaguzi, kisha wakatoka nje ya jengo na kama hiyo haitoshi,
ofisa huyo akiwa na mbwa alikwenda sehemu ya kuegesha magari yenye kesi
na yale ya kawaida na kuanza kufanya ukaguzi, baada ya hapo waliondoka,”
alisema polisi huyo na kuongeza:
“Licha ya mimi kutokuwa na cheo pale,
lakini hili la kutukagua na mbwa, ni kama wametudhalilisha... sisi
ndiyo tunaaminika kwa usalama, leo hii wanatukagua na mbwa. Tena Kituo
Kikuu.”
Hata hivyo, usalama kwenye vituo
vingi ikiwamo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juliusu Nyerere, vilikuwa
chini ya usimamizi na uangalizi wa makachero wa Marekani.
No comments:
Post a Comment