Sharifa Mahmud (27) akiwa mbele ya dawa za kulevya anazodaiwa kukamatwa nazo nchini Misri
SAKATA la Watanzania wawili waliokamtwa na dawa za kulevya nchini
Misri imezidi kuwa na usiri mkubwa, baada ya ndugu zao kushindwa kupata
ukweli juu ya uhai wao na tuhuma zinazo wakabiri.
Akizungumza na Mwanadishi wetu jijini Dar es Salaam
ndugu wa karibu na watuhumiwa hao ambao ni mtu na binamu yake, alisema
kwamba serikali ya Misri imeendelea kuficha ukweli wa suala la ngudu
zake kukamatwa na dawa za kulevya.
"Bado tunahangaika kupata taarifa kamili juu ya maisha ya ndugu
zangu, tumeweza kuwasiliana na ubalozi wa Misri nchini Tanzania wakasema
kwamba hawana taarifa sahihi juu ya suala hilo, tukawasiliana na
Serikali ya Tanzania kupitia ubalozi wake nchini Misri, lakini taarifa
tuliyopata ikatupa utata zaidi"alisema ndugu wa watuhumiwa hao kwa
masharti ya kutotajwa jina lake mtandaoni.
Alisema kwamba "Ubalozi wa Tanzania nchini Misri uliweza kuwasiliana
na Mamlaka zinazohusiana na kitengo cha dawa za kulevya na kukutana na
watuhumiwa hao, ambapo walituwezesha kuzungumza nao kabla hawajapandshwa
Mahakamani lakini baada ya hapo upatikani wa taarifa zao zimekuwa za
siri sana" alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza:. Mpaka
hivi sasa hatuelewi kinachoendelea,mawasilaino yamekuwa magumu ingawa
hatujakata tamaa ya kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini
Misri"
Watuhumiwa hao wenye undugu wa
mtoto wa Mjomba na Shangazi wakazi wa Magomeni na Ilala jijini Dar es
Salaam ni Mbarak Abdallah (28) na Sharifa Mahmud (27), walikamatwa Mei
16 mwaka huu nchini humo wakitoka Jijini Dar es Salaa kupitia Nairobi
nchini Kenya, wakiwa na dawa ya kulevya aina Heroine kilo saba. Baada
ya kukamatwa Mei 18 mwaka huu Ubalozi wa Tanzania nchini Misri uliitwa
kwenda kuwatambua na baada ya kubainika kwamba ni watanzania
walirudishwa rumande baada ya kuzungumza na ndugu zao nchini Tanzania. Mei 26 walipelekwa Mahakamani kwa mara ya kwanza na kurudishwa rumande.
No comments:
Post a Comment