Wastara Juma.
MSANII wa filamu za Kibongo, Wastara Juma hivi karibuni alikataa kuolewa
na kuwa mke wa pili baada ya kupigiwa simu na mwanamke mmoja jijini Dar
akimtaka awe mke mwenzake.
Wastara ambaye hivi sasa yuko Uarabuni kwa ajili ya mapumziko baada
ya kufiwa na mumewe, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’, Januari mwaka huu,
alikataa ofa hiyo
na kusema kwamba kwa sasa hafikirii kabisa kuolewa.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini, mwanamke huyo aliamua kufanya hivyo
baada ya kushauriana na mumewe kuhusu Wastara kuingia katika familia
yao.
“Mwenyewe alisema alishauriana na mumewe na haoni tatizo Wastara
kuwa mke mwenzake kwa sababu imani ya dini yao inaruhusu,” kilieleza
chanzo hicho.
UTHIBITISHO NI HUU
Baada ya kuzinyaka habari
hizo, kama kawaida yate
lilimnyanyulia mkonga mwanamke huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe, akathibitisha kumpigia Wastara.
“Lengo langu lilikuwa zuri
tu, unajua dini yetu ya Kiislamu inaturuhusu kuolewa wanawake mpaka
wanne hivyo niliona ni heri nikae na mwenzangu.
“Halikuwa suala la kukurupuka...tulizungumza na mume wangu na tulishajipanga kwenda kutoa mahari kwao. Nimesikitika sana alivyokataa ila namtakia kila la heri katika maisha yake,” alisema.
“Halikuwa suala la kukurupuka...tulizungumza na mume wangu na tulishajipanga kwenda kutoa mahari kwao. Nimesikitika sana alivyokataa ila namtakia kila la heri katika maisha yake,” alisema.
WASTARA SASA
“Ni kweli
nilipigiwa simu na mwanamke wa huko nyumbani (Tanzania), nilimjibu kama
ninavyokuambia wewe sasa hivi, kwamba sifikirii kuolewa kwa sasa,”
alisema Wastara kwa njia simu alipopigiwa na mwandishi wetu.
No comments:
Post a Comment