DIVA wa kiwango cha juu cha filamu hapa Bongo, Jacqueline Wolper,
ameonekana kujutia historia yake ya kimapenzi baada ya kufungukia
kitendo cha yeye kumuanika kila aliyekuwa akimpenda kwamba kimemtibulia
na sasa amejifunza kutokana na makosa.
Jacqueline Wolper.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Wolper alisema kuwa, kwenye maisha
yake ya huko nyuma ameshajianika akiwa na wapenzi tofauti lakini sasa
atakayempa nafasi kwenye moyo wake hatamuanika ila hilo litakuja baadaye
sana kwani sasa hivi kaweka pembeni kwanza mambo ya mapenzi.
“Sitaki yajirudie yaliyotokea katika maisha yangu ya huko nyuma, hata
hivyo sasa hivi niko bize sana na kazi, mambo ya wanaume nimeamua
kuyaweka pembeni kwanza,” alisema Wolper na kuongeza:
“Sitaki itokee kama ilivyokuwa kwa Dallas ambapo kila mtu alijua alikuwa
ni mtu wangu, kwa sasa nimeamua kutulia kwanza na hata nikimpata
mwingine watu hawatamjua hadi wakati wa ndoa.”
Source:Global publisher
No comments:
Post a Comment