28 April 2013

VITA YA ROMARIO NA PELE YAANZA: PELE AMUITA MWENZIE MJINGA - ROMARIO AMJIBU KWA KUMUITA MPUMBAVU NA MNAFKI

Mshambuliaji wa zamani wa Brazil Romario ameanzisha upya vita vyake na na gwiji wa soka duniani Pele kwa kumuita ni mtu mpumbavu.
Wachezaji hawa wawili wa zamani wa Selecao wamekuwa kwenye ugomvi kwa muda mrefu kufuatia Romario kupinga rekodi za mabao ya Pele mwaka 2007.
"Kuna watu wengi ambao hawajui nini wanataka na mwishowe
wanabaki kushambulia kwa maneno wakati uliopita. Lakini mimi ni mkatoliki na naamini kwamba Mungu siku zote anamsamehe mtu mjinga, hivyo na mie namsamehe mtu wa aina hiyo," Pele alisema Ijumaa.
Na katika kumjibu Pele, Romario aliandika kwenye ukurasa wa Facebook: "Jana, Pele amejibu kuhu kauli yangu maarufu, 'Kimya, Pele ni mshairi". Ni msemo maarufu unaotumika sana, na yeye mwenye amekuwa akiupa sababu ya kukua.
"Kitu cha kipumbavu kabisa alichosema ni kwamba  yeye ni mkatoliki mkubwa. Sidhani yeye ni mkatoliki wa kiasi hicho, kama angekuwa mtu namna hiyo angemtambua mtoto yake kike na angeenda kwenye mazishi.
"Sasa hivi sio tu mshairi, pia ni mpumbavu." - Romario
Miaka miwili iliyopita, Romario alisema Pele anaongea upumbavu mno, baada ya Gwiji huyo wa soka kusema kwamba Romario alikuwa anajaribu kutumia uchawi dhidi ya shirikisho la soka la Brazil kufuatiwa kuachwa kwake kwenye kikosi cha Brazil kilichoshiriki World Cup 1998.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname