Ushosti unaoonekana kuwepo sasa kati ya msanii wa filamu, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ na Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha DTV ambaye ni
mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’
umeibua minong’ono huku baadhi wakidai eti Lulu ana lengo la kumrusha
roho Wema.Hilo limeibuka kutokana na ukweli kwamba, sasa hivi Wema na Penny
haziivi baada ya Diamond kuhamishia penzi kwa mtangazaji huyo na kwamba
kitendo cha Lulu kuonekana ‘close’ sana na Penny ni lazima kitamuuma
Wema.
“Ni ukweli ulio wazi kuwa Wema hawezi kumpenda Penny, lakini
pia kitendo cha Lulu kuwa karibu na Penny ni lazima kitamuuma Wema na
atahisi lao ni moja, inawezekana Lulu kafanya makusudi ili kumrusha roho
Wema,” alisema msanii mmoja wa filamu aliyeomba hifadhi ya jina lake
kukwepa bifu.
No comments:
Post a Comment