Polisi
wa nchini Sweden wamedai kupata dawa za kulevya katika basi
linalotumiwa na mwanamuziki Justin Bieber anapofanya ziara zake za
kimuziki.
Msemaji
wa polisi Lars Bystrom amesema kiwango kidogo cha dawa za kulevya na
silaha moja vimekutwa katika basi hilo wakati polisi walipolivamia
likiwa halina mtu na kuegeshwa katika ukumbi wa Globen mjini Stockholm
ambapo mwanamuziki huyo alikuwa akifanya shoo.
Polisi huyo amekata kutaja aina ya dawa zilizokamatwa akisema zimepelekwa maabara kwa uchunguzi.
Hata hivyo hakuna mtu aliyekamatwa.
No comments:
Post a Comment