Uhuru Kenyatta, anaapishwa rasmi leo huku marais wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakitazamia kuwa miongoni mwa wageni
mashuhuri kwenye sherehe hizo.
Uhuru na mgombea mwenza wake,
William Ruto, walichaguliwa katika uchaguzi wa Machi 4 mwaka jana kwa
zaidi ya kura milioni 6.13 na hivyo kumshinda mpinzani wake Rail Odinga,
aliyepata kura milioni 5.3 .
Uchaguzi huo ulifuatiwa ule wa
Desemba mwaka wa 2007 uliomalizika kwa ghasia za kikabila na kusababisha
zaidi ya watu 1,000 kupoteza maisha na wengine kupoteza makazi.
Kuhusu
sherehe, maofisa wa Serikali ya Kenya, walisema zinatazamiwa
kuhudhuriwa na viongozi kadhaa barani Afrika na kwamba baadhi yao
walianza kuwasili nchini humo tangu jana.
Viongozi hao ni
pamoja na Rais Jakaya Kikwete ambaye ameambatana na maofisa kadhaa wa
Serikali yake.Wengine ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul
Kagame wa Rwanda, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Rais Omar al-Bashir wa
Sudan.

No comments:
Post a Comment