Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekabidhi hadharani kigunia kilichojaa fedha takriban dola 100,000 taslim kwa kundi la vijana, kitendo kilichoibua maswali ni jinsi gani vijana hao watatumia fedha hizo.
Makabidhiano ya msaada huo yalionyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha taifa, huku sehemu kubwa ya jamii ikilaumu tukio
hilo.
Mchambuzi mmoja wa mambo amesema lazima kunapaswa kuwa na utaratibu utakaohakikisha vijana hao wanatumia vipi fedha hizo.
Hata hivyo mmoja wa mawaziri wa serikali ya rais huyo amesema kukabidhi fedha hizo hadharani kunahakikisha ukweli na uwazi.
Rais Museveni alikuwa amewaahidi kuwasaidia kundi hilo la vijana wakati wa kampeni zake mwaka 2011.
Kulikuwa na vigelegele wakati rais Museveni alipokuwa ameshikilia kifuko hicho cheupe kilichokuwa na shilingi milioni 250 kabla ya kukikabidhi kwa kwa mwakilishi wa vijana wa Busoga Youth Forum.