Katika filamu hiyo, Cynthia na Wema wataigiza na staa mkubwa wa Nigeria ambaye hata hivyo kwa mujibu wa kampuni inayosimamia filamu hiyo, jina lake bado ni siri.
Kwa muda mrefu Cynthia Masasi alikuwa akiishi nchini Marekani ambako aliwahi kuonekana kwenye video za wasanii wakubwa wakiwemo T.I, Juvenile, Jazze Pha, Rick Ross na wengine.
Kampuni ya Rimacy Entertainment Group ya Tanzania ndio itakayoifanya filamu hiyo. Kwa mujibu wa mratibu wa mchakato huo Seif Kabelele filamu hiyo ambayo jina lake bado halijawekwa wazi, itazinduliwa Tanzania, Kenya, Uganda, Uingereza na Marekani.
Amesema May 4 kutafanyika usaili wa waigizaji wengine zaidi ya watano watakaoukula shavu kwenye filamu hiyo.
Usaili utafanyika Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Huu ni mchanganuo wa waigizaji wanaohitajika:
•A Girl / 5-8 Years. / Any Ethnicity
•Female / 25-30 Years. / Any Ethnicity
•Male/ 31-40 Years. / Any Ethnicity
•Male / 41-50 Years. / Caucasian
•Male / 18-24 Years. / Any Ethnicity
•Female / 18-24 Years. / Any Ethnicity
•Male / 25-30 Years. / Any Ethnicity
•Female / 25-30 Years. / Caucasian
•Male / 31-40 Years. / Any Ethnicity
•Female / 31-40 Years. / Any Ethnicity
.Female / 51-60 Years./ Any Ethnicity
.Male / 31-40 Years./ Caucasian
No comments:
Post a Comment