WATAALAMU wa masuala ya afya na kilimo
kutoka mataifa mbalimbali duniani, wamebaini mahindi, karanga na mihogo
yenye sumukuvu ni moja ya vitu vinavyochangia saratani ya ini, udumavu
wa mwili na akili kwa watoto.
Ingawa takwimu sahihi hazijapatikana
kuonesha madhara ya kila
nchi kutokana na utafiti hizo kuendelea, tatizo limeelezwa kuwa ni kubwa hasa katika nchi za Afrika kutokana na mfumo mzima wa uzalishaji katika sekta ya kilimo na ukuzaji wa mazao usiozingatia utaalamu.
nchi kutokana na utafiti hizo kuendelea, tatizo limeelezwa kuwa ni kubwa hasa katika nchi za Afrika kutokana na mfumo mzima wa uzalishaji katika sekta ya kilimo na ukuzaji wa mazao usiozingatia utaalamu.
Kutokana na ukubwa wa tatizo, wataalamu
hao kutoka nchi 20, wanakutana jijini Dar es Salaam kwa siku tatu,
kuanzia jana, kutafuta njia madhubuti za kukabiliana na sumukuvu.
Tanzania inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zilizochukua hatua za awali
dhidi ya tatizo hilo.
Akizungumza jana katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi alisema,
“Lengo la mkutano huu ni kuwapa fursa
wataalamu kuja na mikakati itakayoisaidia serikali na sekta binafsi
kupambana na sumu ya aflatoxin kwa kuwa hata hapa Tanzania ni tatizo
kubwa.”
Dk Mwinyi alifafanua kuwa, tatizo kubwa
linaonekana kwenye mazao yanayoathiriwa zaidi na sumukuvu ambayo ni
mahindi, mihogo na karanga na husababisha watumiaji kupata saratani ya
ini na watoto hudumaa akili na mwili.
Alisema pamoja na serikali kupitia
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na sheria ya kudhibiti vyakula
vinavyoingia nchini, lakini sheria pekee haziwezi kumaliza tatizo hasa
ikizingatiwa kuwa Watanzania wengi wanatumia nafaka hizo wakati
zikiendelea kukua shambani bila kuzipima kiwango cha sumukuvu
kinachotakiwa.
Sumukuvu ni aina ya sumu inayosababishwa
na kuvu katika mazao na ingawa haiepukiki katika nafaka, kuna kiwango
kinachopaswa kuwepo na kinapozidi, huleta madhara hayo.

No comments:
Post a Comment