SIKU chache baada ya gazeti la Risasi Jumamosi kutoka na habari iliyoambana na picha zilizopigwa katika chumba cha hoteli zikimwonesha mbunge wa jimbo moja nchini akijivinjari na dada mmoja wa mjini, aibu zaidi imemwangukia binti huyo baada ya picha zake za utupu kuvuja.
Mjasiriamali huyo wa mjini, katika habari hiyo jina lake lilifichwa lakini sasa tunalianika kwa jina moja la Sheila ambaye makazi yake ni Kinondoni jijini Dar.
Habari za moto zilizopatikana kutoka kwa vyanzo makini, vimepenyeza maelezo ya kutosha kuhusu ‘mjasiriamali’ huyo kuwa ni moto wa kuotea mbali kwa vigogo.
Folda lenye picha chafu za dada huyo zilizopigwa katika mikao ya kihasarahasara (haziwezi kuachwa wazi) zipo kwenye dawati la Ijumaa kama ushahidi
source mpekuzi