01 March 2013

MAAJABU........MTOTO WA MIAKA 8 AFUNGA NDOA NA KIZEE CHA MIAKA 61'.Angalia PICHA Tukio zima

Maajabu na laana kubwa imetokea  huko Nchini Zimbabwe ambapo Harusi iliyoshuhudiwa na watu takribani 100 iliyowahusu wanandoa wawili ambapo mume ana miaka 8 na mke kuwa na miaka 61 , ambapo kwa haraka haraka ni sawa tu na mtu na mjukuu wake.
Famila za pande zote mbili zilikubaliana na tukio hilo la kihostoria na tukio hilo kufanikishwa huko Nchini South Africa .


Shangazi wa Mvulana huyo ambaye ndiye mume Bi. Patience Masilela (46), alielezea sababu ya tukio hilo kama ifuatavyo:

"Mizimu walimuamuru kijana kuoa haraka kutokana na ukweli kwamba Babu yake hakubahatika kuoa kwa harusi yenye sharehe kubwa, kwa hiyo alimuamuru mjukuu wake huyo afanye hivyo kwa heshima yake na Ndipo Kijana huyo alipomchagua Helen (61) kuwa Waridi wa moyo wake." Alisema Shangazi huyo.

"Nilishaoelewa na nina watoto watano sasa, lakini nilivyosikia kijana huyu amenichagua ilibidi nikubaliane nae kwasababu yalikuwa ni matakwa ya wazee" alisema Bi. Helen ambaye ni Bi harusi kama anavyoonekana kwenye Picha .

"Nimemuoa Helen kwa matakwa yangu mwenyewe kwasababu nilipenda kufanya hivyo, Nilimchagua kwasababu nampenda na nimefurahi kumuoa, Ila nitakwenda Shule na nitasoma kwa bidii " Alisema mtoto huyo.

Mume wa Bi Helen alikuwa na haya ya kusema  baada ya tukio hilo:
"Sikuona ajabu kwa Mke wangu kuolewa na mtoto huyu wa miaka 8 kwani nilijua kuwa ndicho mizimu wanachotaka, mimi na watoto wangu Tunafuraha na jambo hilo na wala hatuna tatizo lolote na Ndoa yao mpya" Alimalizia Alfred Shabangu (65) ambaye Alikuwa ni Mume wa Ndoa wa Bi Helen.

Wanandoa hao walimalizia ndoa hiyo kwa mabusu Moto moto....!!!

Comments system

Disqus Shortname