27 February 2013

AIBUU..MSICHANA ALIYE SHIRIKI KATIKA VIDEO YA KIDATO KIMOJA ya J.I AMTELEKEZA MTOTO STEND YA UBUNGO


Mrembo  aliyewahi kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva  ukiwemo wimbo wa Kidato Kimoja ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya Silemwe, amedaiwa kumtelekeza mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior  Justine (3).

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika kituo cha 
mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo  aliokolewa na msamaria mwema.


Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa  mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.

“Maya  amezaa na kaka yangu Justine anayeishi Marekani na amekuwa akimjali sana kwa kumtumia fedha za matumizi mara kwa mara. Kisa ni kwamba kaka  alimwambia Maya ampeleke mtoto Bukoba (nyumbani kwa baba wa mtoto)  akasalimie, Maya akakubali lakini akamwambia atapitia kwanza Arusha  (nyumbani kwao) ndipo waende Bukoba.

“Justine akamuelewa lakini kumbe alidanganya, hakwenda Arusha na kuna watu walimuona akiingia kwenye klabu moja hapahapa Dar es Salaam,  wakamjulisha kaka. Sasa alipompigia kumuuliza, akawa anajing’atang’ata,  siku iliyofuata akadamkia Ubungo ili kumsafirisha mtoto kwenda Bukoba  kwa mama yetu (bibi wa mtoto) lakini alitaka kumsafirisha kwa kumtumia  kondakta,”

alisema Monalisa na kuongeza: “Alikubaliana na kondakta  huyo kisha akamwachia namba ya simu ya mama na yake ili waweze  kuwasiliana na kumpokea mtoto huko Bukoba.

Kwa bahati mbaya siku ile yule konda alikuwa hasafiri mpaka siku inayofuatia. Mtoto akaanza  kuhangaika stendi siku nzima bila uangalizi mzuri.

“Bahati nzuri  mama mmoja msamaria mwema akafuatilia na kuonana na huyo konda,  akamuomba namba za mama wa Bukoba kisha akawasiliana naye, kwa kuwa  alikuwa na safari ya kwenda huko siku iliyofuata, akaamua kuchukua  jukumu la kusafiri naye.”

Monalisa alikubali kutoa namba za simu za  msamaria aliyejitolea kusafiri na mtoto huyo, alipopigiwa alikiri lakini aliomba sana asitajwe .

“Mimi kama mzazi iliniuma sana  kumuona mtoto mdogo anahangaika stendi bila uangalizi. Nilishangaa sana  kuona mzazi aliyeingia ‘leba’ anawezaje kumwacha mwanaye mdogo namna ile asafiri mwenyewe?” alisema.


baba  mzazi wa mtoto huyo, Justine aishiye Marekani ambapo alisema: “Jambo  hilo limeniumiza sana. Kwa kweli kama ningekuwa huko nyumbani (Bongo)  ningehakikisha namfundisha adabu huyo mwanamke kupitia sheria. “Nashukuru kusikia kwamba mwanangu alifikishwa salama Bukoba.”

Mama wa mtoto huyo alipopigiwa simu alizua  kioja baada ya kukataa kwamba hajawahi kumuacha mtoto kwa konda Ubungo  na pia akadai eti hana mtoto na wala hajawahi kuzaa katika maisha yake  yote. Wakati tukijiandaa kwenda mitamboni juzi Jumatatu, habari  zilizopenyeza katika chumba chetu cha habari zilisema kwamba mrembo huyo alimpigia simu mama mkwe wake na kumchimba mkwara mzito

Comments system

Disqus Shortname