WAKATI kukiwa na tetesi kuwa lile kundi la muziki wa bongo fleva Pah
One, limevunjika
meneja wa kundi hilo amekana ishu hiyo na kudai kuwa kundi bado
lipo lakini kikubwa ambacho kilitokea ni kutokuelewana ndipo baadhi ya
wasanii walipoamua kusafiri na kubaki wawili na watakaporejea
wataendelea kama kawaida.
Kundi hilo linaundwa na vijana wanne ambao ni Nahreel , Ola, Aika na
Igwee ambao wamekuwa wakifanya muziki wa tofauti ambao unaweza
kuwatambulisha zaidi hata kimataifa.
Hata hivyo meneja huyo alipotakiwa kujitambulisha jina lake alidai huwa
hapendi jina lake litokee kwenye vyombo vya habari