08 January 2013

DOWNLOAD na SIKILIZA WIMBO MPYA wa DI-ACTION ---- MHESHIMIWA HAKIMU




Artist:Di.action.
Song:mheshimiwa hakimu
Produced by: dony blast&bizzo one
Studio:hood voice records&jamvibe records!


 full lyricrs mheshimiwa hakimu!

 

Intro
Yeah!
I say mheshimiwa hakimu
Yeah!
I say mheshimiwa

Verse 1!
Sodoma usije mapema shahidi niropoke ukweli
Uongo umezidisha promo, jamii inakula artificial
Mambo yanakwenda nega vipaji vimepewa sumu,wabovu wapate malisho
Wasanii siku hizi wamechina,wengi wanaabudu mapenzi mitaa imekosa wakala
Cheki aliyevuma enzi zile leo sote tuko jalala
 mheshimiwa hakimu huku kwetu sio kwema  migomo kila tukiamka
Umeshindwa kumziba tobo, unamruhusu akamvunje pita
Ama unapata futari damu ya machizi ikimwagika
Usijifanye hauoni wakati mwangosi amevuta
Ama ilikuwa filamu akacheza scine ya kivita
Aah Mheshimiwa hakimu hili bomu litaleta ufa
Ama litaleta maafa baadaye ndio ligeuke kujuta
Mheshimiwa hakimu na muda umeniambia kimbia
Zile dawa  arvs siku hizi mnaleta bandia
Mwana wangu wa mtaa usichoke kaza kimbia.
Yeah

Corous!!!
Yeah!
I say mheshimiwa hakimu,
Yeah!
I say mheshimiwa,
Yeah!
I say mheshimiwa hakimu,
Yeah!
I say mheshimiwa.

Verse 2!

Mheshimiwa hakimu kaka siku hizi hapigi mishe anasaka maza wa kumlea
Sister ye anakwenda resi mwili amegeuza behewa,wanazama chatu  wanatoka ilimradi mfuko una mapera
Aah mheshimiwa hakimu huku kwetu sio shwari
Tizama wana wa mtaa wanaanguka kwa wali nazi
Fanyeni basi mpango tuokoe hiki kizazi
Ama unaona poa pongezi kwa jinamizi
Ama nikiongea vya msingi kwako vinageuka matusi
Tuache tupige soga na story kumhusu sofi
Aah mheshimiwa hakimu watu wanakacha jinsia,wakiume anajiita dada mwili amegeuza biashara
Hova niongoze vyema nipite ndani ya mstari
Ibilisi ameongeza speed anataka anivue rozari
Aah mheshimiwa hakimu hili swala la udini cheki damu inamwagika
Ama kwako sherehe umwone jirani anazika?


Repeat corous
Yeah!
I say mheshimiwa hakimu,
Yeah!
I say mheshimiwa,
Yeah!
I say mheshimiwa hakimu,
Yeah!
I say mheshimiwa.

Verse 3!
Mheshimiwa hakimu shujaa wangu alivuta akaniacha na majambazi wanaoficha mali huko mbali
Nchi inachezwa kamari,ukidai unachonga sana utamwagiwa tindikali
Ama utauziwa kesi usionekane hata maskani
Kama unabisha poa ulimboka bado ana story
Aah mheshimiwa hakimu kivipi ukiss mlungula
Ama kisa una key corio aende kuzurura
Ama hukumbuki ahadi uliyonipa kabla ya kura
Mheshimiwa hakimu kweli unataka kuniua nasikia unaficha uswisi
Kweili leo nimeamini kura yangu alikula fisi
Ama mnimuache amani nimkamate ibilisi
Hoku mtaa kumekucha, raia walisharauka
Makarau wanazingua hizi nyakati za mashaka
Mheshimiwa hakimu hebu tuache hayo masihara
Acha kuniona fala,kumbuka nchi naidai sa kivipi niache hasira?yeah!

Repeat corous!
Yeah!
I say mheshimiwa hakimu,
Yeah!
I say mheshimiwa,
Yeah!
I say mheshimiwa hakimu,
Yeah!
I say mheshimiwa.

Autro
Yeah!
This is conscious men
Rest in peace mwalimu Julius nyerere,
                       Amina chifupa,
                       Daudi mwangosi
See you when we get there men!
                 Yeah!
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx!

Comments system

Disqus Shortname