Leo asubuhi kumetokea hali ya
kutokuelewana kati ya kocha Roberto Mancini na mchezaji toto tundu Mario
Balotelli kiasi cha kufikia kushikana mashati na kutaka kupigana kama
isingekuwa kuamuriwa na wachezaji wengine. Chanzo cha ugomvi wa wawili
hao kinasemekana ni rafu ya Balotelli aliyomchezea mchezaji Scot
Sinclair katika mazoezi hayo ya kujiandaa na mechi ya FA Cup dhidi ya
Watford.
SOURCE-SHAFIIDAUDA |