Baada
ya kunusurika kufa ndani ya uwanja, hali iliyompelekea kustaafu Kucheza
mpira katika Umri mdogo, Fabrice Muamba ameonesha kipaji chake kwa
sanaa ya kucheza Muziki katika kipindi maalumu cha dansi ‘Strictly Come
Dancing’ kinachorushwa na Televisheni ya
BBC Entertainment.
BBC Entertainment.
Ikiwa
ni miezi kadhaa tangu kustaafu Mpira wa miguu, Muamba mwenye miaka 24
alicheza wimbo maalum wa Christmass ‘The Waitresses’ katika mtindo wa
Salsa huku akipewa sapoti na dansa wa kike maarufu kama Vilani.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Bolton Wanderers na mzaliwa wa Zaire, aliwambia
waandishi wa habari kuwa lengo la yeye kushiriki ni kutaka kufurahi na
kupata faraja, Muamba aliongezea “ ulikuwa ni uzoefu mzuri sana kwangu
na nimefurahia, nilitaka kuonesha ulimwengu upande mwingine kuhusu mimi,
pia ni jukwaa la kuonesha kuwa sasa nafanya vingine”.
Muamba
alimalizia kwa kusema “ Ndio! nakumbuka sana kucheza mpira lakini ipo
wazi sababu ya kwanini sitocheza tena, na kitu muhimu zaidi katika
maisha yangu ni Mke wangu na mwanangu”.
source-moblog