16 July 2014

GARI LA NAIBU WAZIRI MAKALLA LATOLEWA MKUTANONI CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI BAADA YA KUZUKA VURUGU

Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam jana. Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Kwa habari zaidi juu ya sakata hilo tembelea blog hii. PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

1 comment:

  1. hao jamaa wenye virungu akina nani,hivi nchi hii kila mtu akashika kirungu itakalika.hebu watuambie kama hao ni kampuni ya ulinzi inaitwaje na jeshi la police inaijua,naomba majibu!

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname