Hivi karibuni msanii wa Uganda Jose Chameleone ameshindwa kuperform
kwenye show ya nchini Norway baada ya kukosa visa ya kuingia nchini
humo.
Tukio hilo limemfanya promoter aliyeandaa show hiyo ale
hasara na kumuita Chameleone ni mwizi.
Baada
ya promoter huyo kumuita hitmaker wa Valu Valu mwizi, jana ameutumia
ukurasa wake wa Facebook kumjibu promoter huyo ambaye naye amemuita
mbabaishaji baada ya kushindwa kumtafutia visa.
“I
hate promotaz who blame artistes for their amateurism!! The Norway one
is one of them he goes ahead organises a show and fails to get me a
visa, what does he do? He calls me a thief upon his own failure.You
can’t use amateur skills proffessionally!Get a life!”
July
mwaka huu msanii huyo aliingia kwenye mgogoro mkubwa na Mkurugenzi wa
Global Publishers Erick Shigongo aliyemtuhumu kumtapeli fedha hali
iliyopelekea passport yake kushikiliwa na kumfanya aandamane hadi
ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kuidai.