14 October 2012

Rais wa Mauritania apigwa risasi

Rais wa Mauritania


Rais wa 
Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, anapelekwa Ufaransa kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa alipopigwa risasi.


Wakuu walisema rais alijeruhiwa wakati wanajeshi
wa serikali waliokuwa kwenye doria, walipofyatulia risasi msafara wa rais.Kabla ya kuondoka kuelekea Paris, Rais Abdel Aziz alisema kwenye hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni kutoka hospitali, kwamba ameshafanyiwa upasuaji ambao ulifanikiwa.
Inaarifiwa kuwa maafisa wawili wa jeshi wamekamatwa.
Jenerali Abdel Aziz, ambaye anaonekana na mataifa ya magharibi kuwa anasimama dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika eneo hilo, alichaguliwa mwaka wa 2009, mwaka mmoja baada ya kupindua serikali.

chanzo- thisdaymag.blogspot.com

Comments system

Disqus Shortname