18 October 2012

ASKARI MWINGINE AUWAWA KINYAMA ZANZIBAR

Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo katika eneo la Bububu.* *Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani leo, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema mauaji hayo yamesababishwa na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid.

Comments system

Disqus Shortname