18 October 2012

Jah Kimbuteh !The First East African major Reggae Super Star


  Jah Kimbuteh with Roots &Kulture Band
     Muasisi wa mwanzo wa mziki wa hisia kali " Reggae" Afrika ya  Mashariki
Unapouzungumzia mziki wa Reggae au mziki wa hisia kali nchini Tanzania
na Afrika Mashariki
jina la Jah Kimbuteh atuwezi kulikwepa, mwanamziki huyu
mtanzania na
bendi yake "Roots and
Kulture band,aliyoianzisha mwaka 1983.
Jah Kimbuteh ni mwanamziki wa mwanzo wa afrika mashariki kuanza kupiga
mtindo wa Reggae
na kufanikiwa kupata umaarufu ndani na nje ya Tanzania,pamoja na
kufanya maonyesho ya ndani ya
nchini Tanzania, Jah Kimbuteh na bendi yake "Roots and Kulture"
walifanikiwa kufanya ziara za
kimziki katika nchi sita zilizokuwa mstari wa mbele katika ukumbozi wa
Afrika,pia kufanikiwa
kufanya maonyesho katika nchi za ulaya kama vile Norway na Austria.
Mara nyingi mziki wake umekua ukiimbwa kwa lugha ya kiswahili na
kingereza ,na ujumbe uliopo katika
nyimbo zake kwa miaka ya 1980s alikuwa anaimiza sana ukumbozi wa nchi
za kusini mwa Afrika.
baada ya ukombozi huo Jah Kimbuteh aliendelea kutumia mziki wa Reggae
na kuimba katika maswala ya
nayo husu jamii.
Jah Kimbuteh CD zake za mwisho ni "True Democrasy" na "I am The Lion"
baada ya hapo amekuwa kimya
kwa mapumziko ya mda mfupi..lakini washabiki wake wamekua wakijiuliza
lini? mwanamziki huyu muhasisi
Reggae wa Afrika Mashariki atapanda tena jukwaani na kuliendeleza
libeneke..la Reggae? au ?
swali hili atalijibu Jah Kimbuteh mwenyewe ambaye bado tegemeo kwa
washabiki
labda tutafutieni 00255(0)752240938 au 0752240930

Comments system

Disqus Shortname