10 May 2012

HIKI NDICHO KIASI CHA PESA KILICHOPATIKANA KWA AJILI YA MATIBABU YA SAJUKI


Wastara ambae ni Mke wa Sajuki, akiamplfy kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM, amesema imefikia hatua ambayo ni nzuri na wanaweza kuondoka kwenda India japo pesa haijafikia yote.
Pesa iliyokua inatakiwa ni milioni 25 lakini iliyopatikana ni milioni 16 lakini tayari itawawezesha kusafiri kwenda India jumapili au jumatatu ijayo  kwa sababu pesa nyingine bado zinaendelea kukusanywa.
Wataondoka yeye, Sajuki pamoja na kaka wa Sajuki na watakaa India kwa wiki mbili lakini kama kutakua na mabadiliko yeyote atasema na millardayo.com
Mwishoni mwa wiki iliyopita Wastara alithibitisha kuibiwa zaidi ya laki nane kwenye account ya pesa ya simu yake ya mkononi baada ya wajanja wa teknolojia kuzuia pesa zilizokua zinatumwa na watanzania kwenye simu yake, na walifanikiwa pia kuiba pesa zilizokuwemo kwenye account ya Wastara. chanzo-millard ayo

1 comment:

Comments system

Disqus Shortname