13 April 2012

HATIMAYE BABA YAKE LULU NAYE AONGELEA KUHUSU SUALA LINALO MKABILI MWANAYE LULU


Bw. Michael Edward Kimemeta - Baba Lulu
 Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake.Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro

1 comment:

  1. Pole Mr. Michael, lakini nachelea kidogo kusema yafuatayo: Kwanza sintakosea kama nikisema bila shaka hujakuwepo nchini kwa muda mrefu na kama nimekosea basi kwa hili unapaswa kulaumiwa. Si juu ya tukioa la kifo cha ndugu yetu Kanumba la hasha! Bali ni juu ya malezi na makuzi ya mdogo wetu Eliza. Mr. Michael ni muda mwingi vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikilalamika juu ya mwenendo usioridhisha wa Eliza na hata ktk mitandao mbalimbali picha zake zilisizo na staha zimejaa. Lakini sikuwahi kubahatika kusikia sauti yako ikikemea mwenendo huo. Amefanya sherehe kubwa ya kutimiza miaka Kumi na nane ambayo leo hii anaikana huenda ni kutokana na dhahama iliyoko mbele yake. Nina mengi ya kukuambia baba Lulu, lakini naomba niwe na kiasi pamoja na busara niishie hapa, kwani hatujajua bado nini hatima ya mdogo wetu LULU. Namalizia kwa kusema hatukuziba ufa leo inatugharimu kujenga ukuta.

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname