14 April 2012

ANGALIA MAANDALIZI YA TUZO ZA Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012 ZITAKAZO FANYIKA LEO


Kinyang’anyiro hicho ambacho kilianza takriban miezi mitatu iliyopita kilizinduliwa kwa sherehe kali, baada ya hapo kamati ya tuzo ilichagua wana akademi wapatao 50 ambao waliingia kambini siku 2 kwa ajili ya kufanya mchujo wa wasanii ambao walitakiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.
Msanii Nasib Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz anaongoza kinyang’anyiro hicho akiwa anawania tuzo 7 akifuatiwa na msanii Ali Kiba ambaye anamfuatia kwa karibu huku akiwania tuzo 5.
Swali lilopo kwenye vichwa vya watu ni je msanii Diamond ataweza vunja rekodi iliyowekwa na msanii 20% aliposhinda tuzo 5 mwaka jana na pia msanii huyo ataweza kumbwaga msanii mwenzake Ali Kiba??
Picha kwa hisani ya Bongo 5

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname