20 March 2012

KAJALA ARUDISHWA RUMANDE TENA


Msanii wa filamu Kajala Masanja leo asubuhi alipandishwa kizimbani Kisutu kusomewa hukumu lakini hata hivyo hakimu anayeendesha kesi hiyo aliahirisha mpaka siku ya Alhamisi ya wiki hii.
Msanii huyo wa filamu anayesadikiwa kushiriki katika kufuja mali ya umma ambayo ilikuwa chini ya mamlaka ya mumewe aliwasili mahakamani akitokea Segerea ambapo alikuwa amelala rumande tangu
Alhamisi iliyopita.
Bongo5 ilikuwepo mahakamani lakini ilipata upinzani mkali kutoka kwa maafisa magereza na polisi ambao waliweka ulinzi mkali kiasi kwamba hakuna mtu mwingine zaid ya Kajala mwenyewe, Wakili, Hakimu pekee na mwendesha mashtaka walioweza kuingia kwenye chumba cha kesi.
Aidha hata Baba yake Kajala alitolewa nishai na askari aliyekuwa amevaa kiraia akimtaka yeye na watu wengine waliokuja kutoka nje na kufuata utaratibu wa kuingia ndani kumwona kajala mahabusu.
 Baadhi ya watu waliofika mahakamani hapo ni pamoja na baba mzazi mzee Masanja, Mama yake mama Masanja, Producer Lamar, Pennyl na washkaji zake ambao hawakufahamika kwa majina.
Vilio kutoka kwa marafiki hao vilisikika baada ya Kajala kuibuka kutoka chemba ya mahakama akiwa analia na kuzua hali ya taharuki na hofu ya inaweza amehukumiwa tayari. Aidha ilichukua muda kujua kwamba kesi imeahirishwa kwakuwa mawasiliano kati ya chemba na watu wengine yalikuwa yamesitishwa kwa muda kutokana na ulinzi mkali uliopelekea watu wengine wote kubaki nje bila kuingia chumba cha mwendesha mashtaka.
Katika hali ya kushangaza hakuna msanii yeyote wa filamu ambaye alikuwepo katika eneo la mahakama hiyo ya Kisutu.

SOURCE- Bongo 5 blog

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname