Meneja wa klabu ya Manchester United Sir Alex
Ferguson amepuuza kejeli kutoka kwa wakuu wa Manchester City juu ya
uwamuzi wake wa kumsajili tena Paul Scholes aliyetangaza mwaka jana
kustaafu mchezo wa soka.
Mcheza kiungo wa zamani wa klabu ya City na
Arsenal, Patrick Vieira aliliambia gazeti moja katika
mahojiano kua "ni
dalili ya udhaifu".
Lakini Ferguson amewaonya kua ana silaha za kutosha ikiwa mahasimu wake wanataka kuanzisha vita vya maneno.
Aliongezea kusema kua ikiwa ni hali ya
kutapatapa kumrejesha uwanjani mmojapo wa wacheza kiungo bora nchini
Uingereza kwa kipindi cha miaka 20 basi nitakubaliana na dhana yao.
Viera, ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa
maendeleo ya soka katika klabu ya City, aliliambia gazeti la Daily
Telegraph siku ya jumatano kua: Kwake yeye Scholes kurudi uwanjani ni
ishara ya udhaifu na kutapatapa kwa United kumrejesha mchezaji mwenye
umri mkubwa wa miaka 37.
United imeshinda mechi tisa za Ligi kuu wakati
Scholes anashiriki na kutoa sare ya mechi moja. Na kufuatia matamshi
hayo, Ferguson akamjibu Mancini wiki ambapo alimruhusu mchezaji
aliyezusha kasheshe Carlos Tevez.
"Roberto alituandama sisi. Ikiwa ni hivyo nasi tutaucheza mchezo huo huo. Silaha zipo tele.
Ferguson alisema "unaposema tunapatapa, wao
wamemtumia mchezaji aliyekataa kushiriki mechi. Wakati huo Meneja aliapa
kua hatomtumia mchezaji huyo abadan' na aliondoka na kwenda zake
likizoni huko Argentina bila ruhusa ya klabu. Nieleze hayo, Je hilo
tutasema ni kutapatapa?
Carlos Tevez alishiriki mechi ya jumatano
Manchester City ilipoibwaga Chelsea 2-1 kuiweka pointi moja nyuma ya
United zikisalia mechi tisa kuhitimisha Ligi ya Premier ya msimu wa
mwaka 2011/2012.
No comments:
Post a Comment