
Alikiba akisalimia na Lupita Nyong’o

Alikiba akibadilisha mawili matatu na mama yake na Lupita
Lupita na Alikiba wote ni mabalozi wa taasisi ya WildAid inayoendesha kampeni ya kuhamasisha watu kuacha kununua bidhaa zitokanazo na ndovu.

Alikiba akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari
Mastaa hao jana walikutana kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Nairobi Kenya ambao wote walihutubia.
Hitmaker huyo wa Chekecha Cheketua aliungana na familia ya Lupita aliyejizoelea umaarufu kwa kuigiza kwenye filamu ya ’12 Years A Slave’, kubadilishana mawili matatu.

Alikiba na balozi wa Marekani nchini Kenya
Alikiba ameshare picha kwenye Instagram ya Lupita akiongea na waandishi wa habari na kuandika, “WildAid Press Conference Nairobi Kenya @lupitanyongo gracefully and passionately making a statement for a positive change in Elephant poaching.”

Lupita Nyong’o

Alikiba akiongea na familia ya Lupita Nyong’o
Kwenye picha nyingine Kiba ameandika: WildAid Press Conference Nairobi Kenya Nilijiunga Na @lupitanyongo Katika Zoezi La Kutokomeza Ujangili Wa Tembo.”
“Nikikutana Na Mama Dorothy Nyong’o Na Kukubaliana Kufanya Kazi Pamoja Kuaangamiza Ujangili Wa Tembo,” ameandika kwenye picha nyingine.

Naye Lupita Nyong’o alipost picha hiyo juu kwenye Instagram na kuandika:
Elephants can hear more than 5km away. So my whisper must be like a shout at this distance…? #dubiouslogic. Tonight’s gala at @villarosakempin is to raise funds and awareness to ensure that we get to hear from elephants for a long long time. @wildaid #ivoryfree #LNhomecoming #elephants #secretsthatcanbeheard.”
No comments:
Post a Comment