12 February 2016

KWA NINI SOUD BROWN KAFANYA JAMBO LA AJABU KUHUSU MIMBA YA WEMA SEPETU

Jana Mtangazaji wa Clouds alizua jambo Instagram kwa kuandika ujumbe tata kuhusu Wema Sepetu ..
Soudy brown kwenye instagram yake kapost picha ya wema kaandika :
"Pole dada wema sepetu, mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu akupe moyo wa uvumilivu pia ili utoke hospitali ukiwa salama, inshallah kazi yake Mola haina makosa"
Kisha akaweka na hashtag #INASEMEKANAETI

Baada ya Ujumbe huo mashabiki wa Wema Sepetu walilipuka kutaka kujua ukweli wa jambo hilo huku wengine wakimrushia matusi Soudy Brown kwa kushusha ujumbe huo....

Mpaka sasa Wema Sepetu wala watu wake wa karibu hakuna aliyejitokeza na kutoa ufafanuzi kuhusu ujumbe huo wa Wema Sepetu kama ni Kweli ama la

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname