Mnamo
Mei mwaka huu, shirika la ndege la la Etihad linategemea kufungua sehemu mpya
ya mapumziko katika stesheni ya tatu ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abu
Dhabi kwa ajili ya wageni wake wa “Daraja la Kwanza”, wasafiri wenye kadi
maalum za Platinum za Etihad, wasafiri wenye kadi maalum za Platinum kutoka
washirika wa Etihad na wale watakaotumia huduma ya “Makazi” iliyopo katika
ndege zake aina ya Airbus A380. Etihad imewekeza sana katika kutimiza lengo
hili kwa ajili ya wageni wake wa hadhi ya juu wanaopenda huduma zenye viwango
bora zaidi.
Peter
Baumgartner, Afisa Mkuu wa Biashara, alisema: “Huduma hii itakuwa kito katika
taji letu hapa Abu Dhabi, ni nafasi nzuri kuonesha umahiri wetu kwenye ubunifu
na uvumbuzi. Ni muhimu kwetu kuhakikisha msafiri anapata huduma bora kwanzia
uwanjani hadi angani mpaka anaposhuka. Tuna imani huduma na bidhaa tutakazotoa
nje ya ndege zitajizolea umaarufu kama za ndani ya ndege na tunategemea wateja
watafurahia yote tunayowaandalia.”
Sehemu
hii ya mapumziko itapambwa kwa mtindo wa Kiarabu na itaendana na umaridadi na
umahiri uliozoeleka na kuhusishwa na jina la Etihad. Sehemu hii itaonesha
uzoefu na ustadi wa Etihad na jinsi walivyojikita katika kuleta huduma yenye
ukamilifu, kuanzia angani hadi ardhini.
***MWISHO***
Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka
2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni
14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au
limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko
Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika
lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa
zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na
Airbus A380s tano.
Shirika la Etihad pia
limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways
, Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline,
likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin,
Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia
hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta
kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora
zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja
wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com
No comments:
Post a Comment