Taarifa hizo zilieleza kuwa Mke wa Dk. Slaa, Josephine alichukua mkopo wa shilingi milioni 300 katika moja kati mabenki nchini na kushindwa kuirudisha fedha hiyo.
Dk. Slaa ambaye yuko nchini Canada akijiendeleza kimasomo, alikanusha taarifa hizo na kueleleza kuwa yeye na mkewe Josephine hawajawahi kuchukua mkopo katika benki yoyote nchini.
“Nataka nikuambie na uwajulishe Watanzania kwamba wala si mimi Dk. Slaa wala mke wangu, Josephine kwa wakati wowote ule hatujawahi kuchukua mkopo benki,” Dk. Slaa aliliambia gazeti la Mtanzania kwa njia ya simu.
“Tangu nitoke Bungeni sijawahi kuchukua hata senti moja benki, achilia mbali propaganda ya shilingi milioni 300. Hivyo, ni vizuri waliokupa taarifa wakupe undani ni benki ipi nilikopa au Josephine alikopa na ni shilingi ngapi na kwa nyaraka zipi. Na ni vema ukafuatilia benki husika pia kama walikuwambia ni benki gani,” Mwanasiasa huyo mkongwe alieleza.
Dk. Slaa ambaye alitangaza mwaka jana kustaafu siasa, alisema kuwa anapanga kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote walioandika habari hizo.
No comments:
Post a Comment