IKIWA ni siku 10 kupita baada ya mtandao huu kuripoti mgomo wa walimu
katika Chuo cha Kimataifa cha Tanzania (TIU) kilichopo Kimara Stop-Over,
Dar es Salaam, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekifutia leseni chuo
hicho. Walimu hao
waligoma kuingia darasani kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kutolipwa
malimbikizo ya mishahara yao pamoja na kutopewa mikataba ya kazi.
Taarifa iliyotolewa na Profesa Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU kwa
vyombo vya habari imeeleza kuwa, chuo hicho kimefutiwa leseni yake
kutokana na kushindwa kutimiza masharti yaliyobainishwa kwenye leseni
iliyowepewa.
Mgaya ameleza kuwa, chuo hicho kimeanzisha kufundisha programu za
astashahada na stashahada bila ithibati ya mamlaka husika na kuongeza
TCU haitambui program zinazotolewa na chuo hicho.
CREDIT: MWANAHALISI ONLINE
CREDIT: MWANAHALISI ONLINE
No comments:
Post a Comment