Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana ulipendekeza chama
hicho kumfuta uanachama rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kwa
madai kuwa anashirikiana na wapinzani kukihujumu chama hicho.
Kauli
hiyo ya UVCCM ilitolewa jana na mwenyekiti wa Umoja huo Taifa, Sadifa
Juma Khamisi katika kilele cha matembezi ya kumbukumbu ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Sadifa alieleza kuwa endapo CCM haitachukua hatua ya kumfukuza, umoja huo utatumia utaratibu tofauti kumuondoa.
Hata
hivyo, leo Karume alihudhuria sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar na pale
jina lake lilipotajwa na rais Ali Shein, umati uliofurika ulimshangilia
kwa nguvu kubwa. Viongozi wa kitaifa wa Chama cha Wananchi (CUF) akiwemo
makamu wa kwanza wa rais, Maalim Seif Sharif Hamad hawakuhudhuria
sherehe hizo
No comments:
Post a Comment