Stori: Na Makongoro Oging’, UWAZI
DAR ES SALAAM: Gari la kifahari linalodaiwa kuwa ni la Mbunge wa
Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa limezua balaa kufuatia
mwandishi wetu kumpigia simu ya kutaka kumuuliza swali ambalo lilitoka
kwa wapigakura wake kufuatia madai kwamba amelinunua gari hilo kwa
shilingi milioni mia mbili.
Jumapili iliyopita, mwandishi wetu alimwendea hewani mbunge huyo na
kuanza kwa kumpa hongera kwa kununua gari hilo aina ya Toyota Land
Cruiser V8.
Mchungaji: Nenda kwenye pointi.
Mwandishi: Kuna habari kwamba umenunua gari la kifahari wakati uliwahi ‘kumchana’ aliyekuwa mbunge wa jimbo lako…
Mchungaji: (anafoka) Mbona nyinyi waandishi mnafuatafuata habari za
watu? Hamjui kuwa mimi nina vitu vya thamani vingi kuliko hili gari!
Mwandishi: Hapana, hayo ni malalamiko ya wapiga kura wako, wanasema
kwamba wewe uliwahi kumsema aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Iringa, Monica
Mbega kwamba …
Mchungaji: (anafoka tena) Mnataka kuni-intimidate (kunitisha)? Mimi
kuwa na gari hata kama lingekuwa la thamani ya shilingi milioni 500 kuna
ajabu gani? Au mnataka kusema nimehongwa na… (anamtaja waziri mmoja wa
zamani.)
Mwandishi: Mchungaji unakwenda mbali, haya ni malalamiko ya wapiga kura wako. Ungesikiliza kwanza…
Mchungaji: (anafoka zaidi) Hakuna! Ndiyo maana nyie waandishi wa habari mnakufa masikini. Kazi yenu kufuatafuata maisha ya watu.
Simu inakatika, mchungaji akapiga yeye, mwandishi akampa mhariri wake azungumze…
Mhariri: Mchungaji mbona unazungumza maneno mazito sana?
Mchungaji: (akiwa hajui kwamba sasa anaongea na mhariri wa gazeti)
Hakuna, nyinyi hamjui kuwa mke wangu ni mtu mkubwa sana benki ya…
(anaitaja jina). Ana uwezo, tena ana mshahara mkubwa kuliko wa wabunge.
Nina mashamba makubwa mbona hujanipa hongera? Una uhakika gani kuwa hili
ni gari langu?
Mhariri: Ndiyo maana tukakuuliza. Basi kama nimekosea, nisamehe mimi saba mara sabini mchungaji.
Mchungaji: Tena hizo habari mziandike hivyohivyo, wekeni ukurasa wa kwanza kabisa (akakata simu
No comments:
Post a Comment