ALIYEKUWA mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa
imeelezwa kuwa yupo kwenye hali mbaya kifedha na kumfanya ashindwe kulipa pango
za ofisi ya Kampuni yake.
Imeelezwa kuwa kiongozi huyo aliyewahi kushika
wadhifa wa Waziri Mkuu na kujiuzuru kwa kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme
ya Richomond, ameshindwa kulipa kodi ya pango ya kampuni inayodaiwa kuimiliki
ya Alpha Dry Cleaners iliyopo kwenye jengo la PPF Tower.
Taarifa za ndani kutoka kwenye kampuni hiyo
imeeleza kuwa licha ya Lowassa kushindwa kulipa kodi ya pango lakini pia
ameshindwa kuwalipa mishahara wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kipindi cha miezi
miwili.
Kampuni hiyo ambayo ilikuwa miongoni mwa vyanzo
vya mapato vya Lowassa inadaiwa kushindwa kujiendesha kutokana na fedha nyingi
kutumika kugharamia kampeni za uchaguzi urais za Lowassa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari ndani ya
kampuni hiyo, kimeeleza kuwa, Alpha Dry Cleaners tangu Novemba mwaka jana,
haijalipa kodi kwa PPF.
Hivyo PPF imelazimika kuiandika barua ya notisi ya
siku 30 kampuni hiyo kulipa kodi kabla ya hatua zingine hazijachukuliwa ikiwemo
kuondolewa kwenye jengo hilo.
Aboubakary Liyongo ambaye ni Msemaji wa Lowassa,
Aboubakary Lyongo alisema hawezi kulijua suala hilo kwa kuwa ndio kwanza
amelisikia kutoka kwetu na kuomba watafute watu wa Alpha.
“Ndio kwanza nasikia kutoka kwenue kuhusu jambo
hilo ila watafuteni watu wa Alpha watakupeni ushirikiano wa kutosha kutoka kwa
watu hao,’’alisema.
Hata hivyo, gazeti hili liliwasiliana na Lulu
Mengele, ambaye ni Ofisa Habari wa Mfuko wa Pesheni wa Mashirika ya Umma,
alisema hayupo ofisini ila atatoa taarifa baada ya kukutana na wahusika.
“Sipo ofisini lakini hiyo nitazungumza na wahusika
na watanipa jibu ambalo nitakupa,’’alisema Lulu.
Alpha Dry Cleaners ni moja ya kampuni za Lowassa, ilianza
kazi mwaka 1999 ikisimamiwa na Fred Lowassa, ambaye ni mmoja wa watoto wa
Lowassa, kabla ya kuanza kwa AlphaTel pale mtaa wa Ohio, ambapo inaelezwa
kampuni hiyo ya usafi inachukua tenda ya kufua nguo za wafanyibiashara wakubwa
na baadhi ya viongozi wa serikali.
No comments:
Post a Comment