07 January 2016

Barack Obama atokwa na machozi akizungumzia silaha kutokana na ongezeko la watu kushambuliwa

post-feature-image 
Rais Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani. Hii ni kutokana na ongezeko la watu kushambuliwa kwa risasi nchini humo. Kiongozi huyo anayemaliza muhula wake wa pili mwaka huu alisema kwa sasa yeye hatafuti kura.

Obama anataka watu wote wanaouza silaha washurutishwe kuwa wakipekua na kuchunguza historia ya watu wanaowauzia silaha. Kwa sasa, takwa hilo hugusa tu wauzaji silaha waliosajiliwa.

Wale hawajasajiliwa, hutakiwa kuwauliza tu wanunuzi watarajiwa iwapo wamewahi kupatikana na makosa ya uhalifu au kama wana matatizo ya kiakili. Hatua hiyo ya Rais Obama imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wakuu wa chama cha Republican wanaosema inaingilia uhuru wa kikatiba wa Wamarekani

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname